Binti yako mwenye umri wa miaka kumi na nne kwa mfano, anaomba umnunulie gari kama ulivyofanya kwa kaka yake mwenye umri wa miaka kumi na nane. Mara ya kwanza unamwambia utamnunulia atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane kama ulivyofanya kwa kaka yake. Lakini baada ya wiki moja binti yako anakuomba tena kitu kilekile, yaani gari. Utajisikiaje? Utakereka, sivyo? Jinsi utakavyokereka binti yako kukuomba kitu ambacho tayari ameshakuomba, ndivyo Mungu anavyokereka sisi kumwomba vitu ambavyo tayari tumeshamwomba. Ukiomba kitu kwa mara ya kwanza Mungu amekusikia, tayari ameshaandaa malaika wa kukuletea jibu. Unachotakiwa kufanya, baada ya kuomba, shukuru mpaka jibu lako litakapofika. Mungu huthamini zaidi maombi ya kushukuru kuliko maombi ya kuomba. Binti yako anachotakiwa kufanya baada ya kukuomba gari ni kukushukuru mpaka gari yake itakapofika, si kukuomba mpaka gari yake itakapofika.

Your Comment Comment Head Icon

Login